Inawezekana kuuza vitabu/dokumenti zako
fupi fupi au ndefu kwa bei ya rejareja—mtandaoni—kwa wateja waliopo WhatsApp.
Ukiwa na shauku ya kuandika na kuuza maandishi yako mtandaoni, siyo lazima usubiri hadi ujikamilishe kwenye vitu vingi. Mwingine anasubiri mpaka apate kompyuta mpakato (laptop) au nyingine kubwa, ajifunze muda mrefu kuhusu Microsoft Word Office na mengine mengi. Lakini siyo lazima mpaka ufanye hivyo ndipo uanze kuuza maandishi yako mtandaoni.
Uwezo mwingine hupatikana na kuongeza ukiwa njiani kufanya kitu. Kiasi kwamba, kama haujaingia kufanya jambo moja kwa moja, hauwezi kupata mafunuo au uwezo huo.
Mimi nilipoanza, nilitumia simujanja (smartphone) yangu tu, kwa ku-install Apps tatu (3) ambazo nilijifunza namna nzuri ya kuzitumia mwenyewe, na kuanza kupata dokumenti nzuri sana—ndani ya muda mfupi.
Apps hizo ni:
• Microsoft Word Office ( for Android)• WPS• Diary.
Nilitengeneza dokumenti nzurí fupi fupi, ambazo nilizitangaza kupitia WhatsApp kwa kuweka makava ya vitabu kwenye blogu rahisi ya bure—(unayoweza kuifungua mwenyewe ndani ya dakika chache) kwenye jukwaa la blogspot. Link ya posti husika niliituma kwa watu na vikundi vya WhatsApp. Nilianza kupata wateja, na niliuza kwa bei ndogo za rejareja sana.
Wateja wangu niliwaambia wanilipe kwa M-pesa, kisha mimi kuwatumia PDF hizo inbox kwa WhatsApp au e-mail.
Kitabu hiki kitakupa mwongozo mzuri wa kuanzia popote ulipo. Ukiwa na smartphone tu, kifurushi cha intaneti na muda wako fulani maalum wa kuwepo mtandaoni; hakuna litakaloshindikana hata kidogo.
FOMATI YA KITABU: PDF.
BEI YA SASA: TSH 2,500/-
MAHALI PA KUWASILISHA CHANGAMOTO YAKO YOYOTE: Kikundi cha WhatsApp [Simple Online Income Skills].
—————————
___________
Comments
Post a Comment