Mara nyingi mtu kama mimi au mwingine yeyote akifuatwa inbox, na kuona namba ngeni; hupatwa na mshituko fulani.
Kwa nyakati fulani nimekutana na watu wengi ambao kabla haujasema kitu kingine chochote, hususan baada tu ya salamu na utambulisho; anaanza kukujibu kwa taswira ya mtu mwingine ambaye amewahi kumshirikisha au kumwambia kitu ambacho yeye hakukipenda kabisa. Kwa hiyo, kuna ile hali ya kubakia na taswira ya mtu yule wa wakati uliopita.
Hali hiyo, kwa namna moja ama nyingine; inaweza pia kukuzuilia nafasi ya jambo zuri ambalo ungelipata kutoka kwa mtu mwingine au ungemshirikisha—ikiwa ungesababisha mazingira ya amani na utulivu—kwa jumbe zako.
Nimejifunza mambo mengi katika hili, na nikija kwako basi ujue miongoni mwa mambo mazuri nitakayoyaleta kwako ni pamoja na mambo yaliyopo kwenye picha zilizopo hapa chini:
--------------------------
Emmanuel Simple Online Library, School And Creative Designing Point.
--------------------------
Comments
Post a Comment