Rafiki, wateja wengine wa biashara yako au bidhaa na huduma unazotoa, wanapatikana kupitia WhatsApp. Swali linalojitokeza kwenye ufahamu wa watu wengi, wanaoambiwa kauli iliyotangulia hapo juu, ni hili: nawezaje kuwauzia watu waliopo mtandaoni—hasa hasa kupitia WhatsApp? Nafahamu kuna wengine miongoni mwetu, tunafahamu namna ya kufanya hivyo, ndiyo maana kuna vikundi vingi vya WhatsApp, vya watu wanaouza bidhaa mbalimbali. Bidhaa kama nguo, viatu, magari, viwanja, vyombo vya majumbani, vifaa vya umeme, vifaa vya ujenzi na nyingine nyingi. Tunahitaji kuendelea kufahamu mambo mapya, na kubadilishana mawazo juu ya namna nyingine mpya inayoweza kutusaidia kuliteka soko kwa urahisi—kupitia WhatsApp. Tunaweza kukumbushana kuwa: katika suala la kuuzia mtandaoni, kuna bidhaa za aina mbili: 1. Bidhaa halisi zinazoshikika (Physical/Tangible Products). 2. Bidhaa za kidigitali (Digital/ Downloadable Products). • Katika aina ya kwanza, ndipo kuna vitu kama nguo, viatu, magari, vipodozi, vifaa ...
—working with and on graphics, PDFs, audios and videos.