Leo, Chagua Kitabu Unachohitaji Kwa TSH 1,000/-[PDF].
YALIYOMO: (4).
1. ORODHA FUPI YA VITABU VITANO (5) [PDF] VILIVYOLETA MATOKEO MAZURI TANGU TULIPOKUWA TUNAANZA.2. UFAFANUZI NA UTANGULIZI KWA UFUPI KWA KILA KITABU.3. JINSI YA KUPATA KITABU HUSIKA.4. MAHALI PA KUELEZA KUHUSU MAENDELEO, CHANGAMOTO AU SWALI LAKO LOLOTE—KUHUSU MAARIFA YALIYOMO.5. MATANGAZO YETU MENGINE.
____________
1. ORODHA FUPI YA VITABU VITANO (5) [PDF] VILIVYOLETA MATOKEO MAZURI TANGU TULIPOKUWA TUNAANZA.
№1. SASA UTAUZA GRAPHICS ZAIDI: Kupungua kwa changamoto katika kuuza graphics—mtandaoni; WhatsApp imerahisisha. (Kutengeneza graphics kwa smartphone na kuziuza kupitia WhatsApp).№2. SASA INAWEZEKANA KUONGEZA UPATIKANAJI WA WATEJA KUPITIA WHATSAPP: utumiaji wa lebo maalum ni suluhisho zuri—hivi sasa.№3. UNAVYOWEZA KUUZA MAANDISHI YAKO MTANDAONI: Uza dokumenti fupi fupi kwa bei ndogo—utauza sana—mtandaoni.№4. KIPATO KWA MAARIFA YA UZOEFU/TAALUMA YAKO—MTANDAONI: tengeneza na kuuza kwa PDF, audio & video.№5. SEHEMU NZURI YA KIPATO: Andika kwa ajili ya wengine mtandaoni_online typing.
—————————
2. UFAFANUZI NA UTANGULIZI KWA UFUPI KWA KILA KITABU.
№1: SASA UTAUZA GRAPHICS ZAIDI: Kupungua kwa changamoto katika kuuza graphics—mtandaoni; WhatsApp imerahisisha.
Mara nyingi watu wanapenda kila wanapoanza kitu, wafikie kwenye hatua ya juu ndani ya muda mfupi. Pia uhalisia wa wazo hilo huvunja mioyo ya watu wengi, linapoangaliwa kwa kina.
Ungependa kupata maarifa yatakayokupa uwezo wa kuanza kubuni (design), kutengeneza na kuuza graphics kama posters, flyers, business card (softcopy), kalenda, makava rahisi ya vitabu na logo rahisi—kwa smartphone kupitia WhatsApp? Ikiwa jibu lako ni ndiyo, basi ni furaha kubwa leo utapata kitabu; kinachokupa maarifa rahisi ya namna nzuri ya kuanza kuitumia smartphone yako kutengeneza graphics na kuwahudumia wahitaji/wateja wake waliopo WhatsApp.
Utapata pia mwongozo wa App nzuri rahisi kuitumia kwenye smartphone kufanikisha hilo. Ndani ya kitabu, maelekezo yameambatanishwa na picha (screenshot) za hatua zote muhimu.
Wateja wako wanapatikana WhatsApp, wao hutuma maelekezo na picha zao kwa WhatsApp au e-mail. Pia watazipata kazi zao katika fomati za kielektroniki (softcopy) kama: PDF & picha—kwa e-mail au WhatsApp. Wao watakulipa kwa mobile money kama M-pesa, halopesa, Tigo pesa, T-Pesa n.k (ikiwa wapo Tanzania) na utatakiwa kutumia link ya kupokelea malipo kwa intaneti (ikiwa wapo nchi nyingine za nje).
№2: SASA INAWEZEKANA KUONGEZA UPATIKANAJI WA WATEJA KUPITIA WHATSAPP: utumiaji wa lebo maalum ni suluhisho zuri—hivi sasa.
Tulipogundua njia mpya ya kuhifadhi (save) namba nyingi za WhatsApp ndani ya muda mfupi, jambo lililoonekana kusababisha matokeo mazuri sana, ni utumiaji wa lebo maalum kusevu namba hizo.
Kwa mfano, tunaweza kusevu namba 300 hadi 500 kwa siku kwa ajili yako. Pia katika kitabu hiki utafundishwa jinsi ya kufanya hivyo mwenyewe. Kuna namna jambo hili linakwenda kukusaidia kufikia watu wengi waliopo WhatsApp, ndani ya muda mfupi.
Tunaposema lebo maalum, tunamaanisha nini? Na kwa nini utumiaji wa lebo maalum umesababisha upatikanaji wa matokeo mazuri sana?
Lebo maalum zinakuwa hivi; tuchukulie mfano huu: unataka kusevu namba 200, kwenye kikundi cha whatsapp kinachoitwa BIASHARA YA SIMU NA KOMPYUTA. Watu wote (200) wa kikundi hicho, kwa mfumo wetu, watakuwa saved kwa jina la kifupisho cha kikundi hicho yaani BISIKO au BSK. Baada ya kusevu; namba ya mtu wa kwanza itaonekena kama BISIKO 1, wa pili kama BISIKO 2, wa tatu kama BISIKO 3...zitaenda hivi hadi wa mwisho (wa 200) kama BISIKO 200.
Kwenye kitabu kuna maelekezo jinsi ambavyo lebo hizi zinaleta matokeo mazuri kwenye maeneo makuu manne:
1. Kurahisisha zoezi la ku-foward tangazo au ujumbe wako kwenda kwa watu wengi wenye lebo moja, ndani ya dakika chache.2. Kutumia mbinu ya P2P Sales Prospecting—kwa namba nyingi.3. Urahisi wa kupata watakaokuwa watazamaji wa status zako—ndani ya muda mfupi.4. Urahisi wa kuweka mkakati wa kutengeneza uhakika wa wateja wengi tarajiwa wasio na kikomo—kupitia WhatsApp.
———————
№3: UNAVYOWEZA KUUZA MAANDISHI YAKO MTANDAONI: Uza dokumenti fupi fupi kwa bei ndogo—utauza sana—mtandaoni.
Ukiwa na shauku ya kuandika na kuuza maandishi yako mtandaoni, siyo lazima usubiri hadi ujikamilishe kwenye vitu vingi. Mwingine wanasubiri mpaka apate kompyuta mpakato (laptop) au nyingine kubwa, ajifunze muda mrefu kuhusu Microsoft Word Office na mengine mengi. Lakini siyo lazima mpaka ufanye hivyo ndipo uanze kuuza maandishi yako mtandaoni. Uwezo mwingine hutokea na kuongeza ukiwa njiani kufanya kitu. Kiasi kwamba, kama haujaingia kufanya jambo moja kwa moja, hauwezi kupata mafunuo au uwezo huo.
Mimi nilipoanza, nilitumia simujanja (smartphone) yangu tu, kwa ku-install Apps tatu (3) ambazo nilijifunza namna nzuri ya kuzitumia mwenyewe, na kuanza kupata dokumenti nzuri sana—ndani ya muda mfupi.
Apps hizo ni:
• Microsoft Word Office ( for Android)• WPS• Diary.
Nilitengeneza dokumenti nzurí fupi fupi, ambazo nilizitangaza kupitia WhatsApp kwa kuweka makava ya vitabu kwenye blogu rahisi ya bure—(unayoweza kuifungua mwenyewe ndani ya dakika chache) kwenye jukwaa la blogspot. Link ya posti husika niliituma kwa watu na vikundi vya WhatsApp. Nilianza kupata wateja, na niliuza kwa bei ndogo za rejareja sana.
Wateja wangu niliwaambia wanilipe kwa M-pesa, kisha mimi kuwatumia PDF hizo inbox kwa WhatsApp au e-mail.
Kitabu hiki kitakupa mwongozo mzuri wa kuanzia popote ulipo. Ukiwa na smartphone tu, kifurushi cha intaneti na muda wako fulani maalum wa kuwepo mtandaoni; hakuna litakaloshindikana hata kidogo.
—————————
№4: KIPATO KWA MAARIFA YA UZOEFU/TAALUMA YAKO—MTANDAONI: tengeneza na kuuza kwa PDF, audio & video.
Najua una uzoefu fulani kwenye kazi yako. Maarifa hayo kuna watu wengine wanatamani wayapate mpaka sasa. Vilevile pengine wewe ni miongoni mwa watu wenye taaluma maalum; yaani pengine umesomea ualimu wa masomo fulani kwenye kiwango chochote cha elimu, au taaluma nyingine yoyote. Mtandaoni (hasa kwenye WhatsApp) kuna watu wengi sana. Miongoni mwao kuna wateja wako, wengi na wa uhakika; kwa jambo lolote unaloweza kuamua kufundisha hata kwanzia leo.
Kuna namna ya kutumia sehemu fulani ya muda wako kutengeneza PDF rahisi, audio fupi fupi na ukipenda pia kuna namna ya kutengeneza video fupi fupi za bila kutumia kamera kwa kiasi kikubwa. Yaani unatumia picha, na kuweka audio fulani nyuma yake; kwa kufuata mtiririko wa picha zitakazokuwa zinaonekana.
Kitabu hiki kitakupa mwongozo wa namna nzuri na rahisi iliyopo hivi sasa; katika kufunguliwa/kufungua blogu ndogo rahisi ya bure (blogspot) na channeli ya bure youtube. Halafu namna rahisi ya kuunganisha blogu, chaneli na vikundi vya WhatsApp vyenye wanafunzi waliolipia mafunzo yako.
• Blogu itakuwa kama maktaba (kwa sababu kuna mfumo wa kuruhusu watu fulani waliolipia, ndiyo waweze kusoma posti za blogu husika: kuna maelekezo).
• Youtube inakuwa bure (free) kwa ajili tu ya kuweka video fupi fupi zinazotangaza tu kuhusu uwepo wako na kuwapeleka watu kwenye blogu; upande wa posti zinazoweza kusomwa na kila mtu, kabla ya kulipia.
• Vikundi vya WhatsApp, yatakuwa ndiyo madarasa ya kusema na kuelekeza vitu kwa undani, moja kwa moja kwa wanafunzi waliolipia mafunzo—mahali pa kutuma audio, picha/video zenye mambo ya kina, kwenye kozi zako.
————————
№5: SEHEMU NZURI YA KIPATO: Andika kwa ajili ya wengine mtandaoni_online typing.
Hivi sana kuna dunia mbili kwenye dunia hii tunayoishi. Au niseme kuna limwengu mbili. Teknolojia ya habari na mawasiliano imesababisha kuonekane ni kama kuna ulimwengu mwingine kwenye huu tuliopo; yaani ulimwengu wa mtandaoni (Internet/Online World). Ulimwengu halisia (physical world) na ulimwengu wa mtandaoni, wenye mazingira ya picha na vitu vingine vilivyo katika fomati tofauti tofauti za kielektroniki.
Kutokana na sababu hiyo, unaweza kufanya shughuli zako za kuingiza kipato kwenye ulimwengu wowote kati ya hizi limwengu mbili. Kila mtu anaweza kujipima na kuona anaweza ku-fit vizuri wapi. Wateja/wahitaji wa kazi za maandishi mtandaoni wanaongezeka kila siku.
Ukiwa na uwezo wa kuandika vizuri na kwa haraka; kazi nyingi za maandishi mtandaoni, unaweza kutengeneza kiasi kizuri cha pesa. Watu wengi sana wametingwa na wanahitaji kukamilisha kazi nyingi za maandishi.
Kuna watu wanahitaji kusaidiwa kuandika mashairi, risala, hotuba au kusahihisha kazi za wakati uliopita ili ziandane na maudhui fulani ya sasa. Kuna watu wanahitaji wapate vitabu kutoka kwenye audio zilizorekodiwa kwenye semina, mahubiri na mihadhara mingine. Kuna watu wanahitaji kupata maandishi kutoka kwenye simulizi fulani au video.
Kitabu hiki kitakupa mwongozo mzuri wa kutumia smartphone yako kutengeneza dokumenti nzuri, kwa haraka kuliko ulivyodhani. Maarifa yaliyomo humu pia yatakusaidia kujua namna nzuri ya kuboresha uwezo wa kuandika aina tofauti tofauti za kazi za maandishi.
Wateja wako watazipata kazi zao katika fomati za kielektroniki (softcopy) kama: PDF, doc, docx, txt na nyinginezo—kwa e-mail au WhatsApp. Wao watakulipa kwa mobile money kama M-pesa, halopesa, Tigo pesa, T-Pesa n.k (ikiwa wapo Tanzania) na utatakiwa kutumia link ya kupokelea malipo kwa intaneti (ikiwa wapo nchi nyingine za nje).
_______________. __________
4. JINSI YA KUPATA KITABU HUSIKA.
Vitabu vyote vipo katika fomati ya PDF. Kwa hiyo, ukipenda kitabu chochote kati ya hivi, unatoa taarifa ya jina la kitabu husika, inbox kwetu [WhatsApp: 0743 517 138]. Utapewa namba ya malipo. Utafanya malipo. Mara tu baada ya kufanya malipo (Tsh 1,500 @kitabu), kitabu hicho utakipokea inbox kwako (WhatsApp) au ukipenda pia tunakituma kwa baruapepe (e-mail) yako. Kutoa taarifa hivi sasa ingia inbox (WhatsApp) [HAPA].
_______________. __________
5. MAHALI PA KUELEZA KUHUSU MAENDELEO, CHANGAMOTO AU SWALI LAKO LOLOTE—KUHUSU MAARIFA YALIYOMO.
Ili kuwa na wewe katika kila hatua, baada ya kununua kitabu chochote; kuna vikundi vya whatsapp vinavyojulikana kama 'Simple Online Income Skills (SOIS)'.
Katika vikundi hivi, wanaongezwa wale wote walionunua kitabu kimojawapo kati ya hivi. Ili akihitaji kuuliza au kufahamu jambo lingine lolote zaidi, kutoka kwenye maarifa hayo aweze kuuliza. Yaani ni kwa ajili ya kupata maelekezo ya ziada, yanayoweza kuhitajika na kupata suluhisho la changamoto zozote. Na unaweza kuuliza kwa muda wako wowote, unapokuwa na nafasi. Kwa hiyo si kwa ajili ya mfululizo wa vipindi. Bali ni kwa ajili ya kutoa mrejesho au kuuliza maswali yako.
Hakuna ukomo wa muda wa kuwepo kwenye vikundi hivi. Pale utakapotaka kuondoka, upo huru kufanya hivyo pia.
___________
MATANGAZO YETU MENGINE:
——————————
Comments
Post a Comment