Kuna namna nyingi tofauti tofauti katika kuanza au kuendelea kuingiza sehemu ya kipato, kwa kufanya mambo yasiohusisha kukutana ana kwa ana; kati ya mtu na mtu.
Kwa mfano, kuna Apps nyingi Google Play Store. Apps zinazoweza kutumika kufanya kazi mbalimbali kwenye simu janja (smartphone), kazi ambazo wengine hawana muda wa kuzifanya lakini wanahitaji kazi au bidhaa zilizokamilika. Hapa ninazungumzia bidhaa za kidigitali (digital) au zinazoweza kupakuliwa (downloadable) au kutumwa na kupokelewa mtandaoni.
Kwa mfano unapotumia Apps za kutengeneza au kubuni matangazo ya biashara, yaliyo kwenye fomati za PDF au picha (graphics) na kuwapatia wahitaji wa graphics hizo; utakuwa umetengeneza moja ya bidhaa tunazoziita digital products. Unaweza kuwahudumia watu wakiwa mahali walipo —wewe pia ukiwa mahali ulipo, pasipo kukutana ana kwa ana. Wateja wako wanakulipa kwa njia ya mtandao wa intaneti au akaunti za simu za mkononi (mobile money) kama M-pesa, Tigo pesa, Halopesa, Airtel money, T-Pesa na nyingine (ikiwa ni watanzania).
Kwa sababu hiyo, kuna maarifa muhimu yatakayokuongezea uwezo wa kuona mambo mengi unayoweza kufanya kwenye smartphone yako; na yana wateja wanaopatikana WhatsApp. Maarifa haya yapo kwenye audio zilizorekodiwa (mp3) vilevile kuna kitabu PDF; vinapatikana kupitia WhatsApp.
Hapo juu nimejaribu kutolea mfano wa huduma ya ubunifu wa matangazo ya biashara, pia kuna ubunifu wa kutengeneza kalenda kwa kuweka picha za mteja wako. Ni mambo ambayo unaweza kuyafanikisha vizuri kabisa kwa kutumia smartphone yako, ni suala tu la kupata mwongozo sahihi wa maelekezo yanayofaa kukusaidia.
Vilevile kuna utengenezaji wa video fupi fupi rahisi za matangazo—kwa kutumia picha za mteja wako. Kuna kutangaza bidhaa za wengine wanaotafuta wateja WhatsApp (ikiwa hauna bidhaa lakini unaweza kuwafikia watu wengi waliopo WhatsApp—kama nilivyoeleza kwenye kitabu).
Kuingiza Kipato Kwa Smartphone Na Whatsapp.
—••—Hapa utajifunza namna nyingine ya kutumia sehemu ya muda na kifurushi chako cha intaneti, kufanya mambo rahisi ambayo yana wateja wengi wanaopakana WhatsApp—kwenye smartphone yako.—••—Utajifunza kuwa; kuna Apps zinazoweza kukusaidia kufanikisha kazi mbalimbali kwenye smartphone yako; ili kuingiza sehemu nzuri ya kipato chako kwa rasilimali rahisi: smartphone, WhatsApp, sehemu ya muda na kifurushi cha intaneti & Apps za kazi maalumu ambazo wahitaji wa kile unachotengeneza wapo WhatsApp.
BEI YA MAFUNZO:
TSH 3,000; kitabu (PDF) & audio.
Karibu sana rafiki (0743 517 138).
_______________
Comments
Post a Comment