Ukiwa hapo ulipo sasa, unaweza kuandaa daftari/karatasi na kalamu ikiwa vipo karibu. Ili tufanye zoezi dogo litakalokunufaisha vizuri pia, kwanzia leo.
Hapa kuna swali la kila mmoja wetu kujiuliza. Majibu yako ni muhimu sana, ukifuata maelekezo—hapo hapo ulipo. Vilevile mwishoni utapata maoni yangu kama sehemu ya majibu ya swali hili, na kupewa link ya kujiunga kwenye kikundi chetu cha mapokezi [JE, UNANUFAIKA KWA WASAPU?]
SWALI LETU: Wewe unanufaika vipi kiuchumi/kibiashara kupitia WhatsApp?
Au ni mambo gani yanayokusaidia kunufaika kiuchumi/kibiashara unapotumia WhatsApp?
Unaweza kueleza kwa ufupi sana, kwa kadiri unavyoweza; ili kuokoa muda pia. Andika mahali unapoandika au tafakari kwa dakika chache, kwenye ufahamu wako.
______
SWALI LINGINE: Katika kunufaika au kutonufaika huko; je, kuna mambo kadhaa ambayo unahisi kwa namna moja au nyingine, yanakuzuia usinufaike vizuri [kiuchumi/kibiashara kupitia WhatsApp]?
Unaweza kutaja angalau mambo matatu; hapo unapoandika au kutafakari kwa dakika chache kwenye ufahamu wako.
_____________
MAONI YANGU:
Kama umefuata nami hapo juu, kuna majibu umeyapata. Lakini pia maswali haya nilianza kuwauliza watu kupitia WhatsApp, na nikafahamu kuwa: katika kutafuta majibu ya swali hili kuna makundi makuu matatu ya watu—kwa vigezo vilivyotajwa hapa chini:
Kundi №1: Watu ambao hawajaanza kunufaika kiuchumi kupitia WhatsApp; hawana biashara/bidhaa/huduma yoyote wanayotoa kupitia WhatsApp na wanataka kupata jambo rahisi la kuanza nalo.
Kundi №2: Watu ambao tayari wana biashara/bidhaa au wanatoa huduma ambazo wateja wake wengine wanatafutwa kupitia WhatsApp. Hawa wanahitaji kuongeza upatikanaji wa wateja wengi waliopo WhatsApp.
Kundi №3: Watu ambao wananufaika kwa kutengeneza na kuuza bidhaa za kidigitali (Digital/downloadable products)—biashara na huduma ndogo ndogo zisizohusisha ulazima wa kukutana ana kwa ana. Wanaohitaji kuongeza maarifa ya namna nyingine ya kutumia smartphone na Whatsapp tu, kuingiza sehemu ya kipato chao.
_____________
Kwa kuzingatia makundi haya matatu; nilitafuta maarifa yanayoweza kujibu maswali haya kwa kiasi kikubwa na nikayaweka kwenye audio, vitabu vya PDF (softcopy) na kwa kuwaunganisha wanaopenda kujifunza, kwenye vikundi husika vya whatsapp:
1. Simplified Graphic Designing.2. Maximum Sale Via WhatsApp.3. e-Businesses Via WhatsApp.
______________
Maelezo kuhusu programu hizi tatu za maarifa, yametolewa kwenye posti yetu ya Namna nyingine 3 za kunufaika kiuchumi/kibiashara kupitia WhatsApp. Unaweza kuiangalia posti hiyo pia kwa kufungua HAPA [OPEN].
Au jiunge kwenye kikundi chetu cha mapokezi kwa link iliyopo hapa chini:
Au uliza lolote kuhusiana na jambo hili (0743 517 138: kwa WhatsApp, kupiga simu/sms).
__________
__________
MATANGAZO:
.
Comments
Post a Comment