—MTAJI MWINGINE ULIONAO HIVI SASA.
KWA MTAJI WA KIFURUSHI CHA INTANETI NA MUDA WAKO WA ZIADA.
Utakapomaliza kusoma posti hii fupi, naamini utakuwa umefahamu mambo manne, ambayo unaweza kuyafanya hata kwanzia leo na kuona manufaa yake vizuri kabisa. Utaongeza ufanisi wako katika kuitumia simujanja (smartphone) yako na muda wako mzuri wa ziada unapokuwa na kifurushi chako cha intaneti.
Utapata uwezo mzuri wa kuyafanikisha mambo haya mwenyewe na kuongeza sehemu nzuri ya kipato chako cha ziada; kwa kutumia simujanja yako, kifurushi chako cha intaneti na muda wako mzuri wa ziada.
Mambo hayo ni:
1. Kuwatengenezea watu picha [Graphics] za matangazo ya biashara, makava ya vitabu, business cards, logo, mabango ya nukuu, matangazo ya matukio mbalimbali, kalenda na nyinginezo—kwa kutumia smartphone yako; na kuziuza mtandaoni—kupitia wasapu.
2. Kukusanya na kutunza (save) namba nyingi za watumiaji wa Whatsapp; kisha kuziuza kwa watu wanaohitaji namba hizo kwa lengo lao la kuwafikia watu wengi sana ndani ya muda mfupi—ili kutangaza biashara au huduma zao kupitia Whatsapp.
3. Kuandika dokumenti fupi fupi za PDF na kuziuza rejareja kwa watu wengi [mbalimbali] wanaopatikana hivi sasa, kwa urahisi sana kupitia Whatsapp.
4. Kuwafundisha wengine mambo ambayo umekuwa na uzoefu mzuri sana katika kuyafanya au kujifunza.
Nitafafanua japo kwa ufupi, jambo moja baada la lingine.
KUMBUKA:
Simujanja (Smartphone) yako ina uwezo mzuri kabisa wa kukusaidia kufanikisha mambo mengi mno [—kiuchumi au kibiashara na kijamii], hasa unapounganisha au kuhusisha matumizi mazuri ya mtandao huu wa kimataifa [INTERnational NETwork (INTERNET)] kupitia Simujanja (Smartphone) yako.
Napenda kusema jambo hili; inasikitisha sana kuona bado kuna watu wengi sana ambao wanatumia simu hizi na teknolojia hii ya habari na mawasiliano kinyume na manufaa mema, makubwa na mazuri yaliyokusuduwa. Intaneti haikuja ili kuwapoteza watu, ipo kwa ajili ya kuitumia vizuri kwenye mambo mema yanayoweza kukuongezea mwendokasi/ spidi ya kufika kule unakokwenda—katika nyaja mbalimbali za kiuchumi, kibiashara na kijamii.
Katika nyakati hizi tulizo nazo; watu wengi wanaotumia sehemu ya muda wao wa ziada vizuri kwenye teknolojia hii, wanaweza kunufaika vizuri; kuliko mtu mwingine asiyeelewa jambo hilo kwa mtazamo chanya. Watu wengi hivi sasa wanamiliki simujanja (smartphone).
Kuna baadhi ya mambo hautakiwi kuhangaika katika kuyafanikisha. Simujanja (smartphone) yako ina uwezo mzuri kabisa wa kutumika kuyafanya.
Ukiwa mfuatiliaji mzuri, kwa utulivu; unaweza kugundua uwezo wa simujanja (smartphone) yako katika mambo mengi ambayo kwa namna moja au nyingine, umekuwa ukihangaika kuyafanikisha.
Leo ninayo furaha na amani kushirikisha mambo machache tu (manne). Naamini kabisa mambo haya si mageni kwako, bila shaka unayafahamu au umewahi kuyasikia. Hivyo si kwamba ni mambo mapya kwako, ila ni jambo la kuongeza maarifa ya kutusaidia kuongeza ubora wa vile tunavyofanikisha mambo kadhaa—kwa namna nzuri zaidi, siku hadi siku.
UFAFANUZI WA MAMBO HAYA MANNE.
1. Kuwatengenezea na kuwauzia watu picha [Graphics] za matangazo ya biashara, makava ya vitabu, business cards, logo, mabango ya nukuu, matangazo ya matukio mbalimbali, kalenda na nyinginezo—kwa kutumia smartphone yako.
✍️ HAPA
2. Kukusanya na kutunza (save) namba nyingi za watumiaji wa Whatsapp; kisha kuziuza kwa watu wanaohitaji namba hizo kwa lengo lao la kuwafikia watu wengi sana ndani ya muda mfupi—ili kutangaza biashara au huduma zao kupitia Whatsapp.
✍️ HAPA
3. Kuandika dokumenti fupi fupi za PDF na kuziuza rejareja kwa watu wengi [mbalimbali] wanaopatikana hivi sasa, kwa urahisi sana kupitia Whatsapp.
✍️ HAPA
4. Kuwafundisha wengine mambo ambayo umekuwa na uzoefu mzuri sana katika kuyafanya au kujifunza.
✍️ HAPA
Comments
Post a Comment