Emmanuel Kimanisha ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma katika shahada ya kwanza ya ualimu wa sayansi. Yuko mwaka wake wa tatu katika chuo hicho lakini ni mtu mwenye shauku kubwa sana na anayependa kutafuta maarifa ya mambo na vitu mbalimbali ambavyo hutumia muda wake wa ziada kuvifuatilia na kuvifanyia majaribio ya vitendo. Katika kufanya hivyo, anayo shauku kubwa ya kuwa na uwanja mpana zaidi wa kujifunza na kufundisha kwa undani ili kushirikishana maarifa, taarifa na ufahamu wa mambo yote yanayowezekana kueleweka na kufundishika kwake. Miongoni mwa mambo ambayo huyafuatilia kwa muda wake wa ziada ni pamoja na maarifa ya mambo yanayohusu namna ya kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika teknolojia ya habari na mawasiliano—intaneti na mengine mengi yanayohusu nadharia za Electronics na Robotics.
Kuna vitabu vyake miongoni mwa vitabu vingine vidogo vidogo ambavyo ameviandika na kuwashirikisha watu mbalimbali, kwa yale ambayo ameyafuatilia na kuyafanyia majaribio ya vitendo. Vitabu hivyo vitakusaidia kupata mwanga mkubwa kwa kuwa na namna nyingine nzuri unayoweza kuutazama mtandao wa intaneti. Ili kupunguza hata kuondoa kabisa watu wanaotumia mtandao wa intaneti chini ya viwango au nje na manufaa stahiki, katika nchi yetu na bara letu la Afrika .
Intaneti ikitumika kwa uzuri na faida , inaweza kusaidia sana katika kubadilisha maisha yako na ya watu wengine wengi. Utaweza kutambua na kufahamu mambo kadhaa muhimu, ambayo yatakupeleka katika hatua nyingine nzuri ya kutumia intaneti kwa manufaa makubwa zaidi hususan kiuchumi na kijamii. Hata kama haukuwahi kufikiria kutumia intaneti kwa namna yoyote ile kukunufaisha kiuchumi, utaweza kupata mambo yatakayokupa mwanga wa namna ya kuanza.
Kila mtu anaweza kufanya jambo jema na zuri lenye manufaa makubwa kwake na kwa jamii yake, kupitia intaneti. Na ni vyema kutambua kuwa; kule tunakoelekea kutakuhitaji uwe na jukwaa lako mtandaoni kwa sababu intaneti na Electronics zitachukua nafasi kubwa katika uendeshaji wa mambo mengi katika nyanja zote. Hivyo kujiandaa na kuanza kupata uzoefu ni muhimu mno kuliko vile mtu asiyeona mbali anavyofikiri.
Emmanuel Online Gadgets 77 (EO Gadgets 77) inahusika na mambo makuu matatu; kuandika kazi za maandishi za maelezo ya kawaida kwa kuwahudumia hata watu walio mbali kwa kupitia intaneti (Emmanuel Online Typing and Transcription Gadget 7 (—EOTTG 7), Kubuni na kutengeneza graphics mbalimbali (EO Gadgets 77 Designs) na inatarajia kukamilisha usajili kwa ajili ya shule na maktaba za mtandaoni [Emmanuel Online Schools and Libraries (EOSL)] kwa ajili ya kuendelea kushirikisha maarifa na njia mbadala katika uvumbuzi wa mambo ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika intaneti na kwa kugusia nadharia zinazolenga kuonyesha muunganiko unaoelekea kuwepo kati ya intaneti na Electronics (Advanced Electronics and Robotics), ili kukabiliana ipasavyo na wazo lijalo la Intaneti ya Vitu (Internet of Things (IoT)— kutoka katika nchi zilizoendelea, ambalo ni wazo linalokwenda kubadili sura ya intaneti kwa kiasi kikubwa.
Kwa sasa EO Gadgets 77 inajihusisha zaidi na uandishi wa kazi za maandishi na kisha wateja wake kuzipokea katika fomati za kielektroniki (softcopy) popote walipo —(EOTTG) na pia kwa sehemu inajaribu kufanya utekelezaji wa kushirikisha kwa sehemu; maarifa mbalimbali yanayohusiana na mambo tajwa hapo juu (EOSL) ,kwa njia ya intaneti kupitia Blogu ndogo na Makundi ya Whatsapp.
Emmanuel Kimanisha.
emmanuellibraries@gmail.com
Comments
Post a Comment