Bila shaka unafahamu kuwa tukiwa kwenye vikundi mbalimbali vya wasapu; tunaweza kupata namba ya kila mshirika wa kikundi husika, hii ni kwa sababu namba hizi huonekana [kama orodha] unapoziangalia kwenye taarifa za kikundi (group info).
Umewahi kugundua jambo hilo? Katika hilo unatakiwa upate urahisi mkubwa sana katika kuongeza upatikanaji wa wateja wako wengi wasio na kikomo kupitia whatsapp; kwa biashara yoyote uliyonayo.
Kwa mfano, umejiunga kwenye vikundi vingapi vya wasapu?
Hebu tuchukulie umejiunga kwenye vikundi vya wasapu ishirini na tano (25). Kila kikundi ulichopo kina wastani wa washirika mia mbili (200 Participants). Hii ina maana kuwa tayari una namba za wasapu za watu elfu tano (5,000).
Naamini kabisa kwamba; miongoni mwa hao watu elfu tano (5,000) kuna wateja wako wa uhakika; kwa biashara au kitu chochote unachofanya au unachoweza kuanzisha hata leo—mtandaoni au kwenye mazingira halisi (yasiyo ya mtandaoni).
Pengine utaniuliza "hii inawezekanaje?". Pengine umekuwa ukijiunga kwenye vikundi vingi vya wasapu, hata zaidi ya vikundi 25, lakini hauoni matokeo makubwa; katika kuongeza upatikanaji wa wateja wako.
Sababu siyo kwamba hao watu wote hawahitaji kabisa huduma au bidhaa za biashara yako. Sababu ni kwamba kuna jambo moja unatakiwa kujifunza kwa muda huu mfupi; jambo litakalokupa taswira halisi ya wasapu na njia rahisi sana inayoendana na wasapu—katika kutangaza na kushirikisha biashara au huduma zako.
Ukijifunza jambo hili; utagundua kwamba wasapu inaweza kutumika kuandaa wateja wengi wasio na kikomo—kwa biashara yoyote uliyonayo.
Katika kufaidi maarifa ya jambo hili nataka nikupe sehemu ya taarifa sahihi zilizopo kwenye programu hii.
Namba za watu waliopo kwenye kikundi fulani cha wasapu; tunazisevu kwa jina MOJA rahisi la kifupisho.
KWA MFANO; Namba za watu waliopo kwenye kikundi cha wasapu kinachoitwa:
1. AFYA NA BIASHARA; tunazisevu kama ANB (ANB 1 hadi ANB 200).
2. MAHUSIANO YA NDOA; tunazisevu kama MYN (MYN 1 hadi MYN 200).
3. UUZAJI WA USHIRIKA; tunazisevu kama UWU (UWU 1 hadi UWU 200).
4. BIDHAA KUTOKA CHINA; tunazisevu kama BKC (BKC 1 hadi BKC 200).
5. UUZAJI WA GRAPHICS MTANDAONI; tunazisevu kama UGM (UGM 1 hadi UGM 200).
Tunafanya hivyo kwa vikundi vyote unavyojiunga. Tukisevu namba hizo kwa mfumo huo kwenye baruapepe (e-mail) unakuwa na hifadhi kubwa ya kudumu ya namba za wasapu. Pia hata ukiamua ku-left vikundi vyote ambavyo tayari umesevu namba kwa mfumo huo; namba hizo unabaki nazo siku zote [—na zipo wasapu], na unaweza kuamua uzitumie vipi.
Sasa, sisi tunakuelekeza namna nzuri ya kutumia namba hizo kwa namna itakayokuongezea wateja wako wengi [wa uhakika] na wasio na kikomo kupitia wasapu. Kitabu cha maelekezo yote na audio za maelekezo yote vinapatikana kwa wasapu [ni PDF & mp3] kwa bei ya shilingi elfu tano mia tano (Tsh 5,500/-).
KUMBUKA: Maarifa haya yanakusaidia kuandaa wateja wako wengi na wa uhakika kupitia whatsapp; KWA AINA YOYOTE YA BIASHARA ULIYONAYO/ HUDUMA ZOZOTE UNAZOA—KWA NAMNA ZOZOTE.
—•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—
Ikiwa hauna biashara yoyote kwa sasa; ni vyema uanze na utoaji wa huduma rahisi yenye wateja wasioisha mtandaoni—kupitia whatsapp [HAPA].
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
SQFR 777-004: 4—•••—
•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—
Ad: Maarifa Mengi Mazuri Mtandaoni; Mtandaoni ni mahali penye fursa unazoweza kufaidi, ukiwa katika hali yoyote kiuchumi.
•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—
Comments
Post a Comment