—Intaneti ina watu wengi sana tunaoweza kuwafikia kwa urahisi—ndani ya muda mfupi.
Karibu sana ndugu, kwenye posti hii nzuri. Napenda kuitumia nafasi hii, kwa dakika chache, kukumbushana uwepo wa biashara nzuri na huduma nzuri tunazoweza kuzitoa kupitia intaneti. Bila shaka tunafahamu na tunakumbuka kila siku, kuwa intaneti ina watu wengi sana tunaoweza kuwafikia kwa urahisi—ndani ya muda mfupi.
Katika nyakati hizi, wasapu imerahisisha sana upatikanaji wa watu. Ukweli usiopingika kabisa ni huu: miongoni mwa maelfu na mamilioni ya watu wanaotumia wasapu [nchini kwako, barani kwako & dunia nzima], kuna wateja wengi na wa uhakika kwa biashara au huduma yoyote uliyonayo na ile utakayoianzisha leo. Jambo la msingi la kukuletea matokeo mazuri ni kufahamu namna ya kuwafikia na kuwajulisha uwepo wako.
Huduma na biashara hizi, ninazotaka kuelezea hapa [kwa lengo la kukumbushana], ni rahisi pia kuzianzisha ukiwa katika hatua yoyote kiuchumi. Nina maana gani ninaposema hivyo? Ni maana hii: kitendo cha wewe kufika hapa na kusoma posti hii; basi unao mtaji mzuri wa vitu vitatu ambavyo ni:
Simujanja (Smartphone),
Kifurushi cha Intaneti na
Muda wa kuwepo mtandaoni.
Mtaji huu ndio unaweza kutumika kuanzisha na kuendesha mambo ninayotaka tukumbushane hapa chini.
Huduma na biashara nzuri za bila kukutana ana kwa ana [Mtandaoni].
Hapa nitakupa mambo manne kwanza, halafu la tano ni kitabu ambacho kitakusaidia kupata watu wengi—kupitia wasapu; kwa biashara au huduma yoyote uliyonayo na ile utakayoianza, kati ya hizi:
1. Ubunufu Rahisi wa Graphic.
2. Kuuza Maandishi Yako Mtandaoni.
3. Huduma ya kuwaandikia wengine maandishi mtandaoni.
4. Kufundisha jambo ambalo lina manufaa kwa wengine, na una maarifa mazuri, uzoefu au kipaji katika jambo hilo.
Kitabu kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa wateja kupitia wasapu:
5. Upatikanaji wa wateja kupitia wasapu.
UFAFANUZI KWA UFUPI.
1. Ubunufu Rahisi wa Graphic.
→Angalia kwa picha HAPA.
→Pata dokumenti [PDF] ya utangulizi bure kuhusu programu hii, kupitia wasapu. Ipakue kwa link iliyopo HAPA.
FILE DOWNLOAD [PDF]
2. Kuuza Maandishi Yako Mtandaoni.
→Angalia kwa picha HAPA.
Comments
Post a Comment