Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2020

HUDUMA NA BIASHARA NZURI ZA BILA KUKUTANA ANA KWA ANA [MTANDAONI].

—Intaneti ina watu wengi sana tunaoweza kuwafikia kwa urahisi—ndani ya muda mfupi. Karibu sana ndugu, kwenye posti hii nzuri. Napenda kuitumia nafasi hii, kwa dakika chache, kukumbushana uwepo wa biashara nzuri na huduma nzuri tunazoweza kuzitoa kupitia intaneti. Bila shaka tunafahamu na tunakumbuka kila siku, kuwa intaneti ina watu wengi sana tunaoweza kuwafikia kwa urahisi—ndani ya muda mfupi. Katika nyakati hizi, wasapu imerahisisha sana upatikanaji wa watu. Ukweli usiopingika kabisa ni huu: miongoni mwa maelfu na mamilioni ya watu wanaotumia wasapu [nchini kwako, barani kwako & dunia nzima], kuna wateja wengi na wa uhakika kwa biashara au huduma yoyote uliyonayo na ile utakayoianzisha leo. Jambo la msingi la kukuletea matokeo mazuri ni kufahamu namna ya kuwafikia na kuwajulisha uwepo wako. Huduma na biashara hizi, ninazotaka kuelezea hapa [kwa lengo la kukumbushana], ni rahisi pia kuzianzisha ukiwa katika hatua yoyote kiuchumi. Nina maana gani ninaposema hivyo? Ni maana hii: ki...

TUNAPOKUWA MTANDAONI KWA MANUFAA.

Hivi sasa mtandao wa intaneti unakupa watu wengi sana, kwa urahisi. Kwa mfano, hivi sasa Wasapu inakadiriwa kuwa na watumiaji zaidi ya bilioni mbili (more than 2 billion users)  duniani kote, zaidi ya watumiaji milioni 525 katika bara la Afrika (more than 525 million users)  na zaidi ya watumiaji milioni kumi (more than 10 million users) katika nchi ya Tanzania . Najisikia vizuri tunapozidi kutambua na kukumbuka kuwa: wasapu imerahisisha vile tunavyoweza kuwafikia watu. Usiogope kuanzisha biashara au huduma fulani, hata katika mazingira ya mtandaoni, kwa kigezo cha kusema sina watu wa kuwafikia. Miongoni mwa mamilioni ya watu wanaotumia wasapu, kuna wateja wako wengi na wa uhakika; kwa biashara au huduma yoyote uliyonayo, na hata kwa ile unayoweza kuianzisha leo. Hauwezi kukosa wateja miongoni mwao. Usikose kupata maarifa hata ya kuanzisha kitu rahisi cha kuwahudumia huko huko mtandaoni (biashara za bila kukutana ana kwa ana); mfano mzuri ni kubuni Graphics na kuwahudumia w...

TENGENEZEWA BEAT LA MUZIKI—UKIWA POPOTE.

  SAM, ESSAU & EMMANUEL (SEE) MUSIC BEATS ONLINE. Ndugu msomaji wetu wa taarifa hii muhimu. Leo tunakuletea taarifa na tangazo la kukutengenezea biti (beat) za muziki, katika nyimbo mbalimbali za kumsifu na kumwabudu Mungu, lakini pia nyimbo za injili kwa ujumla wake.  Unatengenezewa biti (beat) zuri sana—ukiwa huko huko uliko, na kulipata kwa wasapu au baruapepe (e-mai). Tupo Dodoma, maeneo ya NG'ONG'ONA karibu na kanisa la E.A.G.T. Vilevile tupo mtandaoni; kwa ajili ya wateja walio mbali na Dodoma. MAELEKEZO NA MPANGILIO WA KAZI. 1. Tunafanyaje unapohitaji kutengenezewa biti (beat)? →Tunao wataalamu wazuri katika kutambua mapema na kwa uzuri kabisa mapigo yanayotakiwa kuwepo kwenye beat lako baada ya kusikiliza maelekezo yako. → NJIA RAHISI YA KUTUMA MAELEKEZO YAKO.  • Ikiwa ni mwimbaji binafsi ,  unajirekodi kwa kuimba kawaida [kwa voice notes/recording with Smartphone) kipisi kidogo tu, na kutuma kipisi hicho kwa wasapu ili kisikilizwe na wataalamu wetu kisha...