Maarifa yanayopatikana kwenye kitabu hiki, yanahusisha utumiaji wa rasilimali zinazopatikana pale pale tulipo, na mtaji mdogo sana wa kiasi cha vocha za vifurushi vya intaneti.
Mambo tunayojadili humu ni maarifa ya namna tunavyoweza kunufaika kiuchumi—kupitia WhatsApp na smartphone, kwa kuangalia mambo makuu matano (5) [na jinsi yanavyohusika kikamilifu]:
1. Uwanja wa wateja wengi wasio na kikomo WhatsApp.2. Kifurushi cha bei ya kawaida cha intaneti.3. Simujanja (Smartphone) yenyewe.4. Sehemu ya muda wa kuwepo mtandaoni (online presence) na5. Apps za kufanya kazi rahisi maalumu/ huduma zenye wahitaji (wateja) wanaopatikana WhatsApp.
Hata kama wewe ni miongoni mwa watu ambao hawajawahi kufanya jambo la kuwaingizia sehemu nzuri ya kipato kupitia mtandao wa intaneti; kitabu hiki kinakupa mwongozo mzuri wa kutumia rasilimali zilizotajwa hapo juu, kwa urahisi sana.
Vilevile hata kwa wewe uliye mzoefu wa kufanya mambo mazuri ya kuingiza sehemu ya kipato kupitia intaneti, kitabu hii kinakufaa kwa kuongeza maarifa ya kufanya mambo mengine mazuri zaidi.
Utaweza kutoa huduma ambazo bidhaa zake ni za fomati za kidigitali/kielektroniki (softcopy). Bidhaa ambazo zinawafikia wateja kule kule waliko kupitia WhatsApp, e-mail au kuipakua mahali pengine mtandaoni—kwa kulipia.
Hakuna ulazima wa kukutana ana kwa ana, kati ya mteja na mtoa huduma. Pia wateja wetu wanatulipa moja kwa moja kwa malipo ya akaunti za simu ya mkononi (mobile money) kama M-pesa, Halopesa, Tigo pesa, T-Pesa, Airtel Money n.k; ikiwa wapo Tanzania. Wengine wanaweza kulipa kwa akaunti za benki au link za kupokelea malipo mtandaoni—ikiwa wapo nchi nyingine za nje.
BEI YA KITABU: TSH 2,500
FOMATI YA KITABU: PDF.
IDADI YA KURASA: 55.
NJIA YA KUKIPATA: WhatsApp & E-mail.
NJIA YA MALIPO: M-pesa, Tigo Pesa, TTCL Pesa.
MAWASILIANO: Ili kupata kitabu hiki leo, ingia WhatsApp Inbox kwetu kwa KUFUNGUA [HAPA] INBOX DOOR.
___________________
Comments
Post a Comment